1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Uganda kuzuwia mzozo wa mpaka kuendelea.

13 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZc

Uganda inania ya kuzuwia mapigano ya hapa na pale yaliyotokea hivi karibuni katika mpaka wake na jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo kuingia katika mzozo kamili.

Maafisa wa Uganda wamesema nchi hiyo inalalamika kuwa mashambulizi mawili yaliyotokea yamefanywa na ama wanamgambo wa Kongo, wanajeshi wa serikali ama wapiganaji wa msituni.

Katika tukio la kwanza , raia mmoja wa Uingereza ameuwawa katika shambulio dhidi ya boti linalofanya utafiti wa mafuta katika ziwa Albert. Na tena wiki iliyopita , wapiganaji kadha waliwafyatulia risasi raia na kupora maduka katika mji ulioko katika ardhi ya Uganda karibu na mpaka wa Kongo.