1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Kura zaanza kuhesabiwa Congo

30 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxv

Kura zimeanza kuhesabiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo baada ya raia wa nchi hiyo kujitokeza kumchaguwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia katika kipindi cha zaidi ya miaka 40.

Takriban Wacongomani milioni 25 wamejiandikisha kupiga kura katika marudio ya uchaguzi huo wa rais kati ya rais anayetetea wadhifa huo Joseph Kabila ambaye alikuwa akiongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo iliofanyika mwezi wa Julai na mpinzani wake Jean Piere Bemba mfanyabishara na kiongozi wa zamani wa waasi.

Uchaguzi huo takribana ulifanyika kwa amani licha ya kuwepo kwa taarifa za hapa na pale za vurugu kufuatia kipindi cha kampeni cha mvutano mkali.Mtu mmoja ameuwawa katika fujo za kupinga kuhujumiwa kwa uchaguzi huo hapo jana kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Mvua zilizorotesha kujitokeza kwa wapiga kura wakato wote wa asubuhi kusini magharibi mwa nchi hiyo na kusababisha muda wa kupiga kuongezwa katika baadhi ya maeneo.

Itachukuwa siku kadhaa kabla ya kutolewa kwa matokeo rasmi ya uchaguzi huo.