KINGSTON : Kocha wa Pakistan auwawa kwa kunyongwa | Habari za Ulimwengu | DW | 23.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINGSTON : Kocha wa Pakistan auwawa kwa kunyongwa

Kocha wa timu ya mchezo wa kriketi ya Pakistan Bob Woolmer ameuwawa kwenye chumba chake cha hoteli baada ya kushindwa kwa fadhaa kwa timu yake na wanagenzi Ireland katika michuano ya Kombe la Dunia.

Kocha huyo Muingereza mwenye umri wa miaka 58 amekufa hapo Jumapili baada ya kukutikana akiwa hana fahamu kwenye chumba cha hoteli yake mjini Kingston Jamaica.

Polisi ya Jamaica imesema kifo chake kimetokana na kukosa pumzi kwa kunyongwa kwa mikono na kwamba yumkini kukawa na mtu mmoja au zaidi waliehusika na kifo hicho.

Wachezaji wa kriketi wa Pakistan wamechukuliwa alama za vidole na kuhojiwa na polisi hapo jana.

Kumekuwa na tetesi kwamba kocha huyo alikuwa afichuwe kashfa ya kupanga matokeo ya michuano hiyo pamoja na kamari katika michuano hiyo.

Kifo cha Woolmer ambaye anaonekana kuwa mmojawapo wa kocha mzuri kabisa wa mchezo wa kriket duniani kimetia kiwingu michuano ya Kriket ya Kombe la Duniaya wiki saba inayoendelea kufanyika huko Carribean ambayo fainali itachezwa hapo tarehe 28 mwezi wa April.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com