Kinagaubaga | Masuala ya Jamii | DW | 08.11.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Kinagaubaga

Sikiliza mahojiano ya Mohammed Abdulrahman na Makamu wa kwanza wa rais wa serikali yamapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi ambae pia ni Katibu Mkuu wa CUF kuhusu hali ya kisisa visiwani Zanzibar

CUF’s Sansibar Präsidentschaftskandidat, Seif Sharif Hamad, beim Gespräch mit Journalisten, nachdem der das Formular für seine Kandidatur bei der Sansibar Wahlkommission (ZEC) abholte (5.Juni 2010) Stichwort: Sansibars Präsidentschaftskandidat, Zanzibar Presidential Candidate, Seif Sharif Hamad

Maalim Seif Sharif Hamadi

Novemba 5  visiwa vya Zanzibar viliadhimisha  mwaka wa pili tangu kuundwa serikali ya Umoja wa kitaifa kati ya chama cha  mapinduzi CCM na kile cha wananchi CUF, Hatua hiyo ilitokana na matakwa ya wananchi. Kuundwa kwa serikali hiyo ya  mseto baada ya uchaguzi mkuu uliopita 2010, kulitokana uamuzi wa  wakaazi wa visiwa hivyo katika  kura ya  maoni ilioitishwa kama sehemu ya  maridhiano yaliofikiwa baina ya aliyekuwa  Rais wa Zanzibar wakati huo Amani Karume na Katibu mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Sharif Hamadi.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada