1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga NOEL kinaelekea Kanada

P.Martin3 Novemba 2007

Kimbunga NOEL kimesababisha hasara kubwa katika eneo la Karibik.Zaidi ya watu 300,000 wamepoteza makaazi yao katika mafuriko mabaya kabisa kupata kushuhudiwa jimbo la Tabasco,nchini Mexico.

https://p.dw.com/p/C77J
Malefu ya watu wamepoteza makazi yao katika jimbo la Tabasco nchini Mexico
Malefu ya watu wamepoteza makazi yao katika jimbo la Tabasco nchini MexicoPicha: AP

Rais Felipe Calderon wa Mexico amesema,vikosi vyote vya anga vinasaidia kupeleka misaada kwa watu waliozingirwa na mafuriko.Asilimia 80 ya jimbo la Tabasco limefurika.

Hata visiwani Jamaika,Kuba na Bahamas kimbunga NOEL kimesababisha mafuriko na hasara kubwa.Maelfu ya watu hawana pa kuishi na wanangojea misaada.Hadi watu 120 wamepoteza maisha yao katika eneo la Karibik na wengi wengine hawajulikani walipo.Sasa kimbunga hicho kinaelekea upande wa Kanada.