1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga DEAN kinasonga mbele

P.Martin19 Agosti 2007

Wakazi wa eneo la Bahari ya Karibean wajiandaa kwa kimbunga DEAN.

https://p.dw.com/p/CHjg
Picha ya kimbunga DEAN iliyopigwa na chombo cha Endeavor kutoka angani,Jumamosi mchana,tarehe 8 Agosti
Picha ya kimbunga DEAN iliyopigwa na chombo cha Endeavor kutoka angani,Jumamosi mchana,tarehe 8 AgostiPicha: AP

Shirika la utafiti wa anga la Marekani,NASA limetangaza kuwa chombo chake cha anga “Endeavor“ kitafupisha safari yake na kitarejea nyumbani siku ya Jumanne,ikiwa ni siku moja kabla ya vile ilivyopangwa hapo awali.

NASA imepitisha uamuzi huo kwa sababu ya wasiwasi kuhusu kimbunga DEAN.

Kimbunga DEAN katika eneo la Karibean kimesababisha vifo 9 na sasa kinaelekea Jamaika na Visiwa vya Cayman ambako raia wameshajitayarisha kujifungia majumbani mwao.

Kimbunga hicho kinatazamiwa kufika Mexico katikati ya juma lijalo na matayarisho yanafanywa kuwahamisha watalii kutoka hoteli zilizokuwepo katika maeneo yanayohofiwa kuwa yataathirika.