1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim Jong Un akamilisha ziara ya kihistoria nchini Urusi

18 Septemba 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameondoka Urusi usiku wa kuamkia leo baada ya kukamilisha ziara yake ya nadra ya siku sita ambayo inaonesha imeimarisha mahusiano yake na rais Vladimir Putin.

https://p.dw.com/p/4WS5g
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: Yuri Smityuk/TASS/picture alliance

Katika siku ya mwisho jana Jumapili, Kim alikitembelea Chuo Kikuu cha mkoa wa Primorye kabla ya kuabiri treni yake ya kisasa kuanza safari ya kurejea Korea Kaskazini.

Ziara hiyo ya Kim huko upande wa mashariki mwa Urusi ilianza Jumanne iliyopita kwa mkutano wa kihistoria na mwenyeji wake rais Putin na kisha kuitembelea kamandi ya jeshi la Urusi ya bahari ya Pasifiki. 

Kabla ya Kim kuondoka, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov alisema Moscow itaendelea kuimarisha uhusiano wake na Korea Kaskazini chini ya misingi ya haki na usawa.

Mataifa ya magharibi yamesema ziara ya kiongozi huyo ilikuwa na na dhima ya kujadili uwezekano wa Korea Kaskazini kuipatia Moscow silaha.