Kikosi cha Ujerumani cha olimpiki charejea | Michezo | DW | 15.08.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kikosi cha Ujerumani cha olimpiki charejea

Michezo ya Olimpiki imemalizika Jumapili iliyopita mjini London, lakini timu zilizoshiriki mashindano hayo yanayofanyika kila baada ya miaka minne , baadhi zimeanza kuwasili nyumbani.

Germany's Miriam Welte (L) and Kristina Vogel celebrate their gold medal during the medal ceremony of Women's team sprint in Velodrom at the London 2012 Olympic Games, London, Great Britain, 02 August 2012. Photo: Christian Charisius dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++

Wachezaji wa timu ya Ujerumani waliolakiwa hii leo

Leo(15.08.2012) maelfu ya watu walikusanyika katika bandari kuu ya mjini Hamburg kuilaki timu ya Ujerumani ambayo ilishiriki katika mashindano hayo. Na huko nchini Kenya timu hiyo haikupokelewa kwa shangwe zinazoambatana kila mara timu hiyo inaporejea nyumbani kutoka katika mashindano makubwa kama hayo. Kikosi cha Olimpiki mara hii kinakabiliwa na uchunguzi kutokana na kutofanya vyema katika mashindano hayo.

Maelfu ya watu walikusanyika katika bandari ya mji wa Hamburg, nchini Ujerumani , wakiwalaki wanariadha wa Ujerumani waliokuwa katika timu ya nchi hiyo iliyokuwa ikishiriki mashindano ya Olimpiki mjini London , ambao wamewasili wakiwa katika meli ya kifahari MS Deutschland.

Meli hiyo ilifuatana na kiasi maboti madogo 80 wakati ikiingia katika mto Elbe na kutia nanga katika bandari ya mji ulioko kaskazini mwa Ujerumani wa Hamburg, ambako watu karibu 10,000 walikuwa wakisubiri kwa saa kadha kuwaona wanariadha wao. Ujerumani imeshika nafasi ya 6 katika msimamo wa mavuno ya medali kwa kupata medali 11 za dhahabu, 19 za fedha na 14 za shaba, na kufanya kuwa na medali 44 za jumla.

**FILE**Germany players pose with their gold medals after beating Spain during their men's final field hockey match at the Beijing 2008 Olympics in Beijing, Aug 23, 2008. The national German hockey team was elected 'Team of the Year' in Baden-Baden, Germany Sunday Dec. 21, 2008. (ddp images/AP Photo/Aman Sharma)

Kikosi cha timu ya mpira wa magongo cha Ujerumani kilichonyakua dhahabu

Kwaya ya mjini Hamburg ikivalia kama wavuvi waliimba nyimbo za kitamaduni pamoja na wimbo wa taifa la Ujerumani wakati wanariadha hao wakiteremka baada ya kukaa baharini kwa muda wa siku mbili katika meli hiyo ya kifahari.

Tulikuwa na wakati wa kufurahisha sana , siku tulizokuwamo katika meli hatutazisahau, amesema mchezaji wa kikosi cha mpira wa magongo ambacho kimenyakua medali ya dhahabu katika michezo hiyo ya mjini London Moritz Fuerste. Kwa kweli nashukuru sana kuweza kuishi katika hali hiyo. Kumekuwa na mambo mengi katika michezo hiyo, amesema meya ya jiji la Hamburg, Olaf Scholz, akikiambia kituo cha televisheni cha NDR. London wamefanya kazi nzuri sana. Baada ya kuwasilisha medali zao na kuwapa saini mashabiki, wanariadha hao walitarajiwa kupanda mashua tano zitakazopita katika vijito vidogo katika mji huo wa Hamburg hadi katika jengo kuu la hamashauri ya jiji, ambako kutafanyika dhifa maalum kwa ajili ya wanamichezo hao.

Kenya's David Lekuta Rudisha (456) raise his arms in victory after crossing the finish line ahead of Kenya's Jackson Mumbwa Kivuna (458) and Sudan's Abubaker Kaki Khamis at left during the finals of the Men's 800 meters event of the IAAF Track and Field World Junior Championships held in Beijing, China, Friday, Aug 18, 2006. Rudisha took gold with a time of 1:47.40 minute. (AP Photo/Ng Han Guan)

David Lekuta Rudisha bingwa wa mbio za mita 800 kutoka Kenya

Wakati huo huo huko nchini Kenya kikosi cha wanariadha walioshiriki katika michezo ya Olimpiki kimelakiwa kwa shangwe na wanafamilia na marafiki leo kilipowasili kutoka London , hata ambapo serikali imetangaza kuanzisha uchunguzi kuhusiana na kufanya vibaya katika michezo hiyo. Waziri wa michezo, Paul Otuoma, amesema ripoti kamili kuhusiana na jinsi timu hiyo ilivyofanya , ambapo Kenya imemaliza ikiwa ya 28, ikiambulia medali mbili tu za dhahabu na kujinyakulia jumla ya medali 11, itatolewa rasmi baada ya uchunguzi kukamilika. Mara hii nataka kusema kuwa hatutaficha chochote. Wakati ripoti ikiwa imetayarishwa tutaitoa kwa umma ili ufahamu kile kilichotokea, amesema Otuoma , ambaye alikuwa mjini London wakati wote wa michezo hiyo.

Katika soka , leo Ujerumani inajitupa uwanjani kupambana na Argentina ya Leonel Messi katika mchezo wa Kirafiki. Italia inakwaana na Uingereza.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe / dpae

Mhariri: Othman Miraji