1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kikao cha G8 chafunguliwa rasmi

Mwadzaya, Thelma7 Julai 2008

Kikao cha mataifa manane yaliyostawi kiviwanda G8 kimeanza rasmi mjini Toyako kaskazini mwa Japan.Mkutano huo unawaleta pamoja zaidi ya wajumbe alfu mbili.

https://p.dw.com/p/EXdK
Bendera za mataifa wanachama wa G8


Ajenda kuu ya mkutano huo ni athari za mabadiliko ya hali ya anga,kutimizwa kwa ahadi zilizotolewa na mataifa tajiri katika kikao cha Gleneagles huko Scotland.Hata hivyo mataifa yaliyostawi kiviwanda ulimwenguni yamewaelezea viongozi wa bara la Afrika wanaohudhuria kikao hicho kuwa yanapanga kutoa shinikizo zaidi ili kuiwekea Zimbabwe vikwazo.Kauli hizo zinatokea baada ya uchaguzi uliogubikwa na utata kufanyika nchini Zimbabwe yapata majuma mawili yaliyopita.Rais Robert Mugabe alitangazwa mshindi katika duru ya pili ya uchaguzi iliyofanyika mwezi Juni alipokuwa mgombea wa pekee baada ya kiongozi wa chama cha upinzani Morgan Tsvangirai kujiondoa kwa madai ya visa vya mateso dhidi ya wafuasi wake.Sikiliza taarifa yake Ali Attas kutoka Tokyo,Japan.