1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI:Kiongozi wa jeshi wa zamani akamatwa

12 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBa6

Kiongozi wa zamani wa jeshi la Rwanda Sam Kanyemera amekamatwa kwa kushukiwa kuhusika na jaribio la kuingilia operesheni za polisi.Kulingana na msemaji wa jeshi hilo Jill Rutaremara Jenerali Sam Kaka anazuiliwa na kesi yake inaanza Agosti 17.Kiongozi huyo wa zamani alikamatwa baada ya bunge kumuondolea kinga ya kutokamatwa.

Bwana Kanyemera mbunge wa chama tawala alikuwa mmoja wa viongozi wa kijeshi katika kundi la uasi la wakati huo FPR.Kundi hilo sasa liko madarakani na ndiyo chama tawala cha RPF.Bwana Kanyemera aidha anashukiwa kumsaidia mfanya biashara Assinapol Rwigara aliyefadhili kudni la uasi la wakati huo jambo linalomwezesha kukwepa kuchunguzwa na polisi baada ya watu 3 kupoteza maisha yao pale jingo moja lilipoporomoka mjini Kigali mwezi jana.