1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Kifo cha rais Ghana chaweza kuleta mshikamano wa kitaifa

Ghana imekuwa katika maombolezo tangu jumanne. Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Mchakato wa amani wa nchi za magharibi (WANEP), Emmanuel Bombandey, hali hiyo inaweza kupunguza mfarakano baina ya vyama vya siasa nchini humo.

Opposition presidential candidate John Atta Mills speaks to supporters at his final campaign rally in Tema, Ghana Friday, Dec. 5, 2008. Mills will face ruling party candidate Nana Akufo-Addo and six other candidates in presidential elections on Sunday, Dec. 7, as two-term leader John Kufuor prepares to hand off power in the West African nation. (ddp images/AP Photo/Rebecca Blackwell)

Aliyekuwa rais wa Ghana Atta Mills

Hali ya mapambano miongoni mwa vyama imekuwa hulka inayofahamika katika nchi hiyo. Lakini baada ya kifo cha marehemu John Atta Mills mapambano yanaweza kupungua. Hayo kwa maoni ya wataalam ni hadithi ya mafanikio kwa sababu nchi za bara la Afrika zimekumbwa na vurugu nyingi katika kipindi cha mpito. Mkurugenzi mkuu katika almashauri inayoshughulika na utawala wa kidemokrasia nchini Ghana, Emmanuel Akwetey, alitaja nchi za Rwanda, Malawi na Nigeria ambayo awali zilikabiliwa na machafuko.

Aliongeza kuwa kwa nchi ambayo imekabiliana na misukosuko na kufanya majeshi yashike hatamu ya uongozi, hakupaswi hata kidogo kuachwa bila kiongozi. Aidha, makamu wa rais, John Dramani Mahama aliapishwa kama makamu wa rais masaa chache tu baada ya kutangazwa rasmi kwa kifo cha rais.

Ghana's Vice-President John Dramani Mahama (C) sits after taking the oath of office as head of state, hours after the announcement of the death of Ghana's President John Atta Mills, in the capital Accra, July 24, 2012. Mills, who won international praise for presiding over a stable model democracy in Africa, died suddenly on Tuesday and his vice-president was quickly sworn in to replace him at the helm of the oil, gold and cocoa producer. Mahama, 53, will serve as caretaker president until the elections at the end of the year. REUTERS/Yaw Bibini (GHANA - Tags: POLITICS ELECTIONS TPX IMAGES OF THE DAY)

Rais mpya wa Ghana John Dramani Mahama

Awali raia walikuwa na maswali vichwani mwao juu ya nani atasimama kwenye uchaguzi mwezi Desemba kufuatia kifo cha John Atta Mills. Lakini sasa chama cha NDC tayari kimetangaza kuwa John Dramani Mahama ndiye atagombea urais kwa tiketi ya chama hicho tawala. Hatua ambayo ilionekana kuwa itaimarisha nafasi yake katika kugombea urais kupitia chama hicho kwenye uchaguzi ujao.

Naibu Katibu Mkuu wa NDC George Lawson, aliambia shirika la habari la Reuters kuwa hakukuwa na upinzani wowote kwenye maamuzi hayo na chama hicho kina imani kwa Dramani. Hali hii imeondoa mianya ya kuwepo mivutano na mitafaruku ndani ya chama kuhusu nani awe mgombea wakati huu wa kulelekea uchaguzi.

Bombaney, akizungumza na shirika la habari la IPS, alisema kuwa kufuzu kwa Ghana katika kipindi hicho cha mpito kumetokana kwa ukubwa na taasisi zake imara. Aliongeza kwamba ana imani Ghana itaendelea kuwa na uchaguzi wa amani mwezi Desemba.

Akwetey alisema pia kuwa raia wa Ghana wamepevuka na wamejifunza kutokana na mapambano ambayo wamekumbana nayo awali kwa mfano uongozi wa kimabavu. Kwa hivyo Ghana imeonyesha dunia kwamba inachukulia katiba yake kama kitu cha maana.

Kofi Owusu ,mwandishi wa habari aliyetuzwa na Msimamizi katika kituo cha redio cha Ultimate mjini Kumasi , alieleza hali ya kisiasa kabla ya kifo cha marehemu Mills kama yenye ukali. Wakati huo, watu walikuwa wakifikiria tu kuhusu atakayeshinda uchaguzi huo ujao.

Lakini Bombaney amesema kuwa Ghana kumpoteza rais wake itakuwa kama kumbusho kwa wananchi juu ya utambulisho wao wa aina moja na kuzuia vyama pinzani kurudi katika makabiliano makali ya awali .

Owusu pia aliambia IPS kuwa tayari viongozi wengine wameanza kuitazama msiba huo kama fursa ya kuimarisha umoja wa kitaifa.

Bombandey amesema, wabunge tayari wameonyesha kwa ukubwa hali ya umoja. Kila chama kimeonyesha mshikamano na serikali na pia familia inayoomboleza. Kwa maoni yake, kuanzia sasa, kutakuwa na mazungumzo ya kiheshima baina ya vyama pinzani ambayo pia itawezesha mazungumzo mazuri zaidi kuhusu mambo yenye umuhimu kwa nchi.

Mwandishi: Trizer Ochieng/IPS
Mhariri: Sudi Mnette