1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kifo cha Boris Yelzin cha gonga vichwa vya habari

24 Aprili 2007

Kifo cha rais wa zamani wa Urusi Boris Jelzin na uchaguzi wa rais wa Ufaransa Mei 6 kati ya Sarkozy na Royal, ndio mada kuu zilizochambuliwa na wahariri wa magazeti ya leo ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/CHT9

Bila shaka Boris Jelzin,alikua ndie kigogo imara katika kipindi cha mageuzi nchini Russia baada ya enzi ya vita baridi.Yeltzin alifariki jana dunia akiwa na umri wa miaka 76 ikibainika kutokana na maradhi ya moyo.

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani, alimpongeza marehemu Jelzin kuwa ni “mpigania-uhuru” na ‘rafiki wa kweli wa Ujerumani`.Lakini kwa jicho la hali ilivyo hivi sasa huko Russia,gazeti la RHEIN-NECKER-ZEITUNG linalochapishwa Heidelberg, laandika:

“Boris Jelzin alikuwa mcheza muziki wa mwisho wa rock ‘n’ Rolle ‘ katika Ikulu ya Russia (Kremlin).Na huo ndio upande wa sifa zake njema.Jelzin alikua pia dikteta wa kujiamini binafsi,lakini mcheshi.Akionesha wakati mwengine alievinjari kweli na mkakamavu kama alipokipandia kifaru kuzuwia kuangushwa madarakani kwa Mikhail Gorbatzschow….

Pia alipalilia rushua na kuitosa Russia mnamo miaka ya 1990ini mara mbili kuwa dola lililofilisika likiomba-omba.Kwamba hayo yote yalitokea sababu ni yeye Yelzin.”

Gazeti la WIESBADENER KURIER limeamua kumlinganisha marehemu Boris Yelzin na mrithi wake wa madaraka -rais Putin.

“Hakuwa Yelzin bali mfuasi wake Putin alieanza kurejesha arkabu za saa nyuma na kukaribisha tena udikteta wa kisoviet.Badala ya kutawala vigogo vya halmashauri kuu ya chama kama zamani,anatawala sasa jasusi wake wa zamani…

Mtu aweza kthubutu kusema marehemu Boris Yelzi alikata zaidi pingu za mfumo wa utawala wa kisoviet kuliko anaejiita mdemokrati Putin.”

Likifuata nyayo hizo hizo ,gazeti la KÖLNISCHE RUNDSCHAU laandika:

“Makusudi Putin haendelezi pale alipoachiwa bali anarejesha arkabu za saa nyuma kabla wakati wa Jelzin.

Amefuta mageuzi takriban yote ya mtangulizi wake-uhuru wa magazeti na amezuwia kuvunjwa kasi kwa idara za usalama na ujasusi nchini.Nadharia iliotanda hivi sasa nchini Russia ni kuwa kipindi cha (Jelzin) 1991-1999 Russia ilitawaliwa vibaya.

Hatua zote za kuelekea mfumo wa uchumi wa soko huru na kufungua milango zaidi ya ushirika na wasaidizi wan chi za magharibi inaonekana ni awamu ya udhaifu wa Kremlin enzi za Yelzin.

Likitukamilishia mada hii,gazeti la LANDESZEITUNG kutoka Lüneburg,linamuona marehemu Yelzin ndie aliefungua mlango ulitosa Russia katika hali yake ya hivi sasa:

ALI: Dola hili la Russia linalotawala kimabavu linaruhusu wapinzani wa serikali nchini kula mkomoto.Wakosiaji-serikali huuliwa na wauaji-mshahara….Urithi aliouacha Jelzin umerahisisha kurejea kwa Russia katika enzi za zamani za udikteta….Kwahivyo, mfuasi wake Putin hakuwa na taabu kutekeleza nadharia zake za kuirejesha Russia kuwa dola la kimabavu.”

Likitugeuzia mada gazeti la DIE WELT linalotoka Berlin, linauchmbua uchaguzi wa kiti cha rais wa Ufaransa.Laandika:

“Wafaransa tayari sasa wameleta mafanikio makubwa.Wamewafunza darasa wafuasi wa mrengo wa kulia wenye siasa kali kwa kuwakataa.

Wamekipiga kumbo chama cha kikoministi na kukigawa vipande vinapnde na wameamua kuleta mabadiliko.

Watetezi 2 waliosalia (Zarkozy na Royal) wanabidi sasa kuania kura za mrengo wa kati .

Hii itaongoza kila mmojawao atabidi kuregeza kamba ili kuwavutia.Nani kati yao atafaulu ni vigumu kusema.Kinyume na duru ya kwanza ya uchaguzi,duru hii ya pili itakua ya kusisimua zaidi.”

Gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINE kutoka Erfurt, linachambua nafasi za ushindi za hasimu wa bibi Royal:Nicholas Sarkozy:

“Sarkozy hangependa sasa kusikia uchunguzi wa maoni ushamtawaza yeye kitini kama mshindi.Kwani, hii itawafanya wafuasi wake wadhani ameshashinda na hawataenda kwa wingi kumpigia kura katika duru ya pili nay a mwisho.Sarkozy amewaita wahamiaji nchini Ufaransa ni aina ya majabazi ambao anataka kuwazuwia kupiga kura.

Kwa matamshi kama hayo Sarkozy aliekuwa hadi punde hivi waziri wa ndani,amewafurahisha wafuasi hadi milioni 3.8 wa siasa kali za mrengo wa kulia.”