1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiev. Waandamanaji wapinga sheria ya rais.

5 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCP

Maelfu ya waandamanaji wameingia mitaani katika mji mkuu wa Ukraine Kiev wakipinga dhidi ya amri kutoka kwa rais Viktor Yushchenko kulivunja bunge.

Wengi wa waandamanaji hao walikuwa wakipepea bendera za rangi ya buluu za chama kinachounga mkono Russia cha waziri mkuu Viktor Yanukovich.

Wakati huo huo , wabunge wamekutana wakipinga amri hiyo ya kulivunja bunge na kutoa wito wa kufanyika uchaguzi wa haraka. Rais ametoa amri hiyo siku ya Jumatatu baada ya mvutano wa miezi kadha wa kugombea madaraka na waziri mkuu.