1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV: Viongozi wa Ukraine wajadiliana

4 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCe

Wafuasi wa viongozi wawili wa Ukraine wamejazana nje ya majengo ya bunge huku rais Viktor Yuschenko mfuasi wa sera za kimagharibi na waziri wake mkuu Viktor Yanukovisch mfuasi wa sera za Urusi wakifanya mazungumzo kuhusu mzozo wa kisiasa uliowazamisha viongozi hao katika ushindani wa madaraka.

Ni siku moja tu tangu rais Yuschenko alipotoa agizo la kuvunjwa bunge la Ukraine na kuitisha uchaguzi wa mapema.

Yanukovisch amesema kuwa hatakubali amri hiyo ya rais Yuschenko na amelitaka bunge kukiuka amri hiyo.

Kamisheni ya ulaya imewataka viongozi hao kufikia suluhisho kwa njia ya amani.