KIEV: Mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine waendelea | Habari za Ulimwengu | DW | 07.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KIEV: Mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine waendelea

Rais wa Ukraine, Viktor Yuschenko, na waziri mkuu, Viktor Yanukovich, walikutana jana kwa mazungumzo lakini suluhisho la kung´ang´ania madaraka kati yao halitarajiwi kupatikana hivi karibuni.

Hapo jana watu takriban 3,000 walikusanyika katika uwanja wa uhuru mjini Kiev, kumtaka rais Yuschenko ajiuzulu. Wafuasi wa waziri mkuu Yanukovich wameahidi kutofanya maandamano wakati wa Pasaka lakini wameapa kuendelea na maandamano baadaye kumshinikiza rais Yuschenko ang´atuke.

Rais Yuschenko alizusha mzozo kati yake na waziri mku Yanukovich wakati alipolivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa mapema ufanyike mwezi ujao baada ya kuwalaumu wabunge kwa ukiukaji wa katiba.

Waandamanaji wameieleza hatua ya rais Yuschenko kuwa uvunjaji wa sheria

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com