KIEV: Chama cha Yuschenko chakataa kujiunga na serikali ya mseto | Habari za Ulimwengu | DW | 05.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KIEV: Chama cha Yuschenko chakataa kujiunga na serikali ya mseto

Chama cha rais wa Ukraine Victor Yuschenko kimeamua kubakia nje ya serikali ya muungano na wapinzani wake na badala yake kitakuwa upande wa upinzani.

Msemaji wa chama cha Our Ukraine amesema atamuomba rais Yuschenko awaondoe mawaziri wa chama hicho walio ndani ya serikali ya waziri mkuu Victor Yanukovic.

Mazungumzo kati ya chama cha Our Ukraine na muungano wa Yanukovic yaliyodumu muda mrefu yamegonga mwamba kwa sababu ya tofauti ya maoni juu ya hali ya baadaye ya Ukraine. Yuschenko anataka kuilekeza Ukraine kwa mataifa ya mafharibi, huku Yanukovic anaunga mkono uhusiano wa karibu na Urusi.

Hata bila kuungwa mkono na chama cha Our Ukraine, Yanukovic ana wingi wa wabunge takriban 240 katika bunge lenye wabunge 450.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com