1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kibaki akataa kutia saini mswada wa kukandamiza vyombo vya habari

23 Agosti 2007

Mswada wa sheria mpya ungelihatarisha mafaniko ya demokrasia nchini Kenya asema rais Kibaki

https://p.dw.com/p/CB1o
Mwai Kibaki
Mwai KibakiPicha: AP


Rais Mwai Kibaki wa Kenya amekataa kutia saini mswada wa sheria juu ya vyombo vya habari.Rais Kibaki amesema mswada huo unahatarisha demokrasi .

Kama rais huyo angetia saini mswada huo na kuwa sheria, sheria hiyo ingezipa mahakama uwezo wa kuwalazimisha waandishi habari kufichua vyanzo vya habari zao.

Rais Kibaki amesema katika tamko kwamba mswada huo ni tishio kwa mafanikio ya demokrasia nchini Kenya.