KHARTOUM: Wanavijiji washambuliwa katika jimbo la Darfur magharibi ya Sudan | Habari za Ulimwengu | DW | 03.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM: Wanavijiji washambuliwa katika jimbo la Darfur magharibi ya Sudan

Watu wenye silaha kutoka chama cha waasi cha vuguvugu la ukombozi wa Sudan SLM ama Sudan Liberation Movement, wamekuwa wakivishambulia vijiji katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan. Mashambulizi hayo dhidi ya wanavijiji, ni kufuatia mapigano na kundi jingine la waasi katika eneo hilo. Umoja wa Afrika umesema kuwa kwa uchache watu 11 waliuawa katika mapigano hayo katika kijiji cha Gereida ambako kunapatikana pia kambi kubwa ya wakimbizi wapatao 130,000.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com