KHARTOUM : Raia 30 wameuawa katika jimbo la Darfur | Habari za Ulimwengu | DW | 11.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM : Raia 30 wameuawa katika jimbo la Darfur

Watu wenye silaha waliopanda farasi wameshambulia lori lililopakia dawa na misaada mingine ya kiutu katika jimbo la Darfur,nchini Sudan na wamewaua kiasi ya raia 30.Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa,baadhi ya wahanga hao walipigwa risasi na wengine walitiwa moto wakiwa hai.Wanamgambo wa Kiarabu wanaojulikana kama Janjaweed wanashukiwa kuhusika na shambulio hilo.Umoja wa Mataifa na mashirika yanayotoa misaada ya kiutu,yamelazimika kuwaondosha wafanyakazi wake wengi kutoka Darfur kwa sababu hali ya usalama inazidi kuwa mbaya katika eneo hilo.Lakini serikali ya Sudan,mara kwa mara imepinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililoidhinisha kupeleka vikosi vya Umoja wa Mataifa na polisi kulinda amani katika jimbo la Darfur.Khartoum inasema hiyo ni kama kuwa na vikosi vya kikoloni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com