Khartoum. Mwenyekiti wa AU asema hakuna haja ya majeshi kutoka nje ya Afrika. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Khartoum. Mwenyekiti wa AU asema hakuna haja ya majeshi kutoka nje ya Afrika.

Mwenyekiti wa umoja wa Afrika , Alpha Oumar Konare, amesema kuwa wanajeshi kutoka mataifa ambayo si ya Afrika hawatahitajika kuwa sehemu ya jeshi la umoja wa mataifa na umoja wa Afrika katika jimbo la Sudan la Darfur.

Katika taarifa kufuatia mkutano na rais wa Sudan Omar al – Bashir mjini Khartoum , Konare amesema kuwa amepata ahadi nyingi za uchangiaji wa jeshi hilo kutoka mataifa ya Afrika.

Serikali ya Sudan inapinga wanajeshi kutoka nje ya bara la Afrika kushiriki katika jeshi hilo lililoimarishwa, ambalo litaundwa na wanajeshi 20,000 wa kulinda amani pamoja na maafisa 6,000 polisi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com