1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM: Mwanachama wa zamani wa janjaweed aikosoa serikali ya Sudan

Mwanachama wa zamani wa kundi la wanamgambo la janjaweed ameilaumku serikali ya Sudan kwa kulidhamini kundi hilo, linalolaumiwa na Marekani kwa kufanya mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa makabila yasiyo ya kiarabu katika jimbo la Darfur.

Mwanamume aliyejitambulisha kwa jina la Ali, ametoa matamshi hayo wakati alipohojiwa na shirika la habari la BBC.

Jana Umoja wa Ulaya uliitolea mwito serikali ya Sudan ikomeshe machafuko yanayoendelea kuzidi huko Darfur lakini haukutishia kuiwekea vikwazo Sudan ili kuilazimisha ikubali wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wapelekwe Darfur kuchukua nafasi ya majeshi ya Umoja wa Afrika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com