1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khartoum. Juhudi za kuitaka Sudan kukubali kuwekwa kwa jeshi la kulinda amani Darfur zaendelea.

14 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAC

Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Negroponte amekutana na maafisa wa Sudan jana katika kile kinachoelezwa kuwa ni juhudi za mwisho za kuishawishi serikali ya Sudan kukubali jeshi la umoja wa mataifa la kulinda amani katika jimbo la Darfur.

Ziara ya mwanadiplomasia huyo mwandamizi inakuja wakati katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa anaimani kuwa vikwazo kadha katika njia ya kutanzua mzozo huo vitaangaliwa na jeshi la umoja wa mataifa lenye wanajeshi 20,000 litawekwa hivi karibuni.