1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM: Holmes azuiliwa kuzuru kambi ya wakimbizi

Mratibu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa,John Holmes amesema,amezuiliwa kutembelea kambi ya wakimbizi,magharibi ya Sudan.Holmes akiwa katika ziara yake ya kwanza katika jimbo la Darfur,aliwaambia waandishi wa habari kuwa mlinzi wa kijeshi kwenye kambi ya Kassad iliyo Kutum, kaskazini ya Darfur,alimzuia kuitembelea kambi hiyo.Amesema,tume yake hapo awali,ilipewa idhini ya kuitembelea kambi hiyo na sasa serikali ya Khartoum imearifiwa kuhusu kile kilichotokea. Akaongezea kuwa walipoanza kuondoka,mlinzi mmoja alimnyangánya mpigapicha wa Umoja wa Mataifa kanda yake ya kamera.Mwaka jana pia,Sudan ilimzuia Jan Egeland,aliekuwa mtangulizi wa Holmes,kuizuru kambi ya wakimbizi.Egeland ndio alisaidia kuligutusha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa Darfur.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com