1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM : 30 wauwawa katika shambulio Dafur

Katika jimbo la vurugu nchini Sudan la Dafur takriban raia 30 wameuwawa na watu waliokuwa na silaha wakiwa wamepanda farasi ambao walilishambulia gari lililokuwa limebeba misaada ya madawa na ile ya faraja.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema baadhi ya wahanga walipigwa risasi wakati wengine walitiwa moto wakati wakiwa hai. Wanamgambo wa Kiarabu wanaojulikana kama Janjaweed wanatuhumiwa kuhusika na shambulio hilo.Hali inayozidi kuwa mbaya huko Dafur imeulazimisha Umoja wa Mataifa na mashirika ya misaada kuwaondowa wafanyakazi wao wengi.

Serikali ya Sudan mara kadhaa imelikataa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye kutaka kuwekwa kwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Dafur kwa kusema kwamba kikosi hicho kitakuwa na sawa na kile cha ukoloni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com