Kenya yapata katiba mpya
5 Agosti 2010Matangazo
Wakenya wamepiga kura kuunga mkono rasimu ya katiba mpya, baada ya kura ya maoni hapo jana. Matokeo hayo yanaipa ushindi kuara ya NDIO wa asili mia 67. Viongozi wa kambi iliyokuwa ikiipinga katiba hiyo mpya wameyakubali matokeo wakisema watashirikiana na wakenya wote kwa kuwa wengi wameamua.