1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Mwanasiasa mkongwe Martin Shikuku afariki dunia

23 Agosti 2012

Kenya inaomboleza kifo cha mwanasiasa mkongwe Martin Shikuku aliyefariki hapo jana baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya saratani.

https://p.dw.com/p/15vMb
Kenya inaomboleza kifo cha Martin Shikuku
Kenya inaomboleza kifo cha Martin Shikuku

Shikuku amefariki akiwa na umri wa miaka 79 akipokea matibabu katika Hospitali ya Hurlingham Nairobi.Shikuku alikuwa mbunge wa eneo la Butere Magharibi mwa Kenya hadi mwaka 1997,lakini harakati zake katika mapambano ya kupigania Uhuru ni jambo ambalo halitosahaulika katika fikra za Wakenya.

Saumu Mwasimba amezungumza na Aliyekuwa makamu wa rais wa Kenya bwana Moody Awori ambaye ametoka mbali kisiasa pamoja na mwanasiasa huyo mkongwe na kwanza anaeleza mambo yatakayokumbwa kwa Martin Shikuku.

(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Saumu Mwasimba

Mhariri: Othman Miraji