Kenya: Maandamano ya kupinga nyongeza ya Mishahara kwa wabunge
14 Mei 2013Matangazo
Wabunge nchini humo wanataka tume inayoshughulikia mishahara ya watumishi wa umma iongeze mishahara yao kutoka elfu 532,000 hadi 850,000. Wabunge hao wa Kenya wanasema kima walichoekewa ni kidogo sana kukidhi mahitaji yao.
Hata hivyo tume hiyo imesema haitabadilisha msimamo wake huku ikitupilia mbali vitisho kutoka kwa wabunge hao waliosema wataifuta kazi tume hiyo iwapo matakwa yao hayataridhiwa.
Mwandishi wetu wa Nairobi Reuben Kyama yuko katika maandamano na kwanza anatueleza hali ilivyo kwa sasa.
Mwandishi Amina Abubakar
Mhariri Yusuf Saumu