1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: dimba lastawi

Isa Omok4 Desemba 2007

Dimba kenya linatazamiwa sasa kustawi:busati la kisasa litatandazwa uwanjani na mfadhili wa Ligi apatikana.

https://p.dw.com/p/CWlH

Harambee Stars, timu ya Taifa ya Kenya, imefunga safari kuelekea Tanzania kwa kombe la CECAFA-kombe la Afrika mashariki na kati ikiandamana na kocha wake Jacob Mulee.

Kenya, itafungua dimba jumamosi hii na wenyeji Taifa Stars- Tanzania.

Kabla “Harambee Stars” kuondoka Nairobi,ziliibuka habari za kupendeza kwa mashabiki wa soka nchini Kenya.Kwanza, FIFA ikiwa sehemu ya mradi wake wa dala miliomni 70 kwa Afrika,itajengewa uwanja wa kisasa wa artificial pitch.Pili,kampuni la michezo la Afrika Kusini-Super-Sport International,litakuwa mfadhili rasmi wa ligi ya Kenya.Uchambuzi wa Isa omok mnasimuliwa na

Mapatano na kampuni la Afrika Kusini “SuperSport International” kuwa mfadhili wa Ligi ya Kenya kuanzia mwakani, yalitiwa saini Novemba 24 na yakasifiwa kua ni ya kihistoria na klabu mbali mbali za ligi ya Kenya-premier League.

Makamo-mwenyekiti wa KPL-Kenya Premier League Gerald Chege aliarifu kwamba kitita hasa cha fedha kitakacholipwa klabu bado hakijaafikiwa lakini kitajulikana pale msimu mpya utakapoanza hapo februari mwakani.

Alisema lakini, klabu zitakazo shiriki katika Ligi hiyo ya Kenya, huenda zikatia mfukoni kitita cha kati ya Kenya Sh. Milioni 2.5 na milioni 3 na hilo ni posho kubwa kwa klabu ambazo zikiishi kwa ruzuku tu.

Mradi mwengine utakaolitia jeki dimba la Kenya, ni ule uliotangazwa na FIFA unaogharimu dala milioni 70 kwa Afrika.Chini ya mradi huu Kenya itafaidika kwa kujengewa busati la kuchezea dimba la kisasa kabisa la “artificial pitch.”

Uwanja huo unagharimiwa chini ya mradi wa FIFA wa kombe la dunia 2010 utgharimu Shilingi za Kenya milioni 42 na utatandazwa katika uwanja wa Nairobi City Stadium,unaochukua mashabiki 15.000.

Uwanja huu ulijengwa na serikali ya kikoloni ya uingereza mnamo miaka ya 1920 na ndio wa kwanza jijini Nairobi kabla ule uliojengwa na wachina wa Nyayo National Stadium unaochukua mashabiki 35.000.Mnamo miaka ya 1980 uwanja mwengine wenye kusheheni mashabiki 65.000 wa Moi International.

Chini ya mradi wa FIFA-shirikisho la kabumbu ulimwenguni, viwanja vyote vya Taifa vya dimba vya wanachama 53 wa kanda ya Afrika isipokuwa Afrika Kusini, wenyeji wa kombe lijalo la dunia 2010.hii ni kuhakikisha kwamba kila nchi barani Afrika,inajipatia sehemu yake ya keki ya Kombe la dunia la kwanza barani Afrika-kwa muujibuwa Ashford Mamelodi-afisa wa maendeleo wa FIFA kwa bara la Afrika.

Katibu mkuu wa shirikisho la dimba la Kenya (KFF) sammy Obingo amesema Kenya inataka kusahau misukosuko yake ya karibuni na kuangalia usoni.Sasa aliongeza Obingo,

“Tunatakla kuitembeza Kenya kuwa mahala pa kutembelewa na timu za Ulaya zitakazokuwa zinaelekea katika kombe la dunia 2010.”

Misukosuko ya dimba nchini Kenya iliongoza serikali kuiingilia kati na kulivunja shirikisho la dimba la Kenya na nafasi yake kuunda Halmashauri ya mpito kuendesha dimba nchini.

Kutia mkono wake kwa serikali katika shughuli za dimba la Kenya, kuliifanya FIFA kuifungia Kenya kushiriki katika dimba la kimataifa .

FIFA ikapeleka Kenya wajumbe wake kusaidia kutatua mizozo iliolikumba dimba la Kenya mna serikali ikarudi nyuma.