1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KENNEBUNK PORT-MAINE:Bush, Putin wakubaliana

3 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmA

Rais George Bush wa Marekani na mgeni wake Vladmir Putin wa Urusi wamesema kuwa watashirikiana katika kutatua mzozo wa mpango wa nuklia wa Iran.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wao huko Kennebunkport, Rais Bush, alisema kuwa ana imani Urusi itaunga mkono katika kutuma ujumbe wa tahadhari kwa Iran kupitia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Lakini viongozi hao walishindwa kuondoa tofauti zao juu ya mapngo wa Marekani wa kuweka makombora ya kujihami katika nchi za Poland na Jamuhuri ya Czech.