Karzai aomba jumuia ya kimataifa kusaidia kuhusu wataliban
21 Desemba 2007Matangazo
KABUL:
Rais wa Afghanistan-Hamid Karzai, amesema kuwa ukarabati wa nchi yake, kwa uchache, utachukua mda wa miaka mingine 10. Katika mahojiano na gazeti la ujerumani,Karzai ametilia mkazo umuhimu wa kuwepo nchini mwake kwa jeshi la Ujerumani kwa lengo la kurejesha utulivu nchini humo. Aidha ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua dhidi ya waTaliban pamoja na maficho ya magaidi yaliyoko nje ya nchi hiyo.