1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karbala.Washia wataka Saddam anyongwe mjini Karbala.

10 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCu4

Muwakilishi wa kiongozi mkuu wa Washia Ayatollah Ali al-Sistani ametoa mwito rais wa zamani wa Iraq Saddam Husein ananyongwa katika mji mtukufu wa Karbala.

Sheikh Ahmed al –Safi, akizungumza wakati wa sala ya Ijumaa huko katika Zawiya ya Imam Hussein, amesema, angependelea zaidi kuona Saddam Husein ananyongwa kati ya zawiya hizo mbili.

Karbala ni mmoja kati ya mji mtakatifu wa Washia, unaokusanya pia makaburi yaliyojengwa kwa dhahabu yenye kuashiria kumkumbuka Imam Hussein na Imam Abbas.

Hata hivyo maelfu ya Wassuni nchini Iraq, na pia rais wa Misri Hosni Mubarak wameonya kuwa endapo hukumu ya Saddam Hussein itatekelezwa, kunaweza kukasababisha maafa zaidi nchini humo.

Licha ya Jumuiya ya kimataifa kulaani kutekelezwa kwa hukumu hiyo, waziri mkuu wa Iraq ambae na yeye pia ni Mshia Nuri al-Malik ameelezea haki ya Iraq katika kutekeleza hukumu hiyo na kwamba itatekelezwa mwishoni mwa mwaka huu.