Kanzela M erkel azuru Greenland | Masuala ya Jamii | DW | 17.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Kanzela M erkel azuru Greenland

Akifuatana na mwenyeji wake waziri mkuu wa Danmark,Kanzela wa Ujerumani alijionea jana kwa macho yake jinsi barafu inavyoyayuka haraka huko Northpol na athari zake kwa mazingira.

Angela Merkel

Angela Merkel

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani, anazuru hivi sasa Greenland.Kwavile athari za mabadiliko ya hali ya hewa huko zaonekana dhahiri-shahiri-Kanzela Merkel jana alizuru Northpol kujionea kwa macho yake sura ya mambo.Akatoa huko mwito kwa walimwengu kutunza mazingira yao.

Kanzela Merkel alifika huko Northpol kwenye m ilima ya barafu inayoyakua kwa kupanda kwa hali ya ujoto ulimwenguni akifuatana na mwenyeji wake waziri-mkuu wa Denmark Anders Rasmussen pamoja na waziri wa Ujerumani wa mazingira Sigmar Gabriel.

Kanzela Merkel akasema:

“Nimevutiwa kupita kiasi na mandhari.Nimevutiwa halkadhalika, na hadithi zinazosimulia juu ya kuyayuka barafu na nini athari zake.

Kwa wavuvi, matokeo yake yafurahisha lakini kwa upande mwengine, kina cha bahari kinapanda na pia ujoto.Tena kinapanda haraka zaidi kuliko sehemu nyengine yoyote duniani.Ndio maana hapa mtu aweza kujionea uzuri zaidi mabadiliko ya hali ya hewa.”

Hiyo ndio sababu iliomtia shime Kanzela Angela merkel kufunga safari na waziri wake wa mazingira Gabriel hadi Greenland ilioko chini ya mamlaka ya denmark.

Kwani kujionea mabadiliko ya hali ya hewa papo hapo kunastahiki juhudi ya ziara hadi huko, ila zilizotolewa na Upinzani nyumbani ujerumani kwamba sera zake za mazingira ni jina tu,amekanusha hayo Kanzela Merkel.

Aliongeza,

“Naamini kuwa inatupasa maswali muhimu ya kisiasa kuyabainisha wazi kwa wananchi.Yatupasa kuwaonesha watu ili waweze kuyatia maanani.Kujionea binafsi hali ya mambo ilivyo papo hapo,hakujamdhuru yeyote,bali kutanutufaisha Hata mwenyeji wake waziri mkuu Rasmussen anatuilia mkazo juhudi za kutunza mazingira.

Kwani, hii si mara ya kwanza anaongoza viongozi wa nchi nyengine kujionea kwa macho yao kinachopita huko kwenye milima na ya barafu ya Greenland.Hapo kabla aliandamana huko na waziri mkuu wa Itali Romano Prodi au pia rais wa Tume ya Ulaya na waziri mkuu wa zamani wa Ureno, Jose Manuel Barroso.

Copenhagen, mji mkuu wa Danmark ndio kituo 2009 cha mkutano wa UM juu ya mazingira.Na ni shabaha ya waziri mkuu Rasmussen, kuona mapatano yanayofuatia yale ya Kyoto yanafikiwa kwa njia ambayo, nchi zitakazo shiriki zinachangia barabara kupunguza ujoto hewani na kuchafua mazingira yetu.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com