1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Merkel akutana na Waziri Mkuu wa China

Admin.WagnerD1 Juni 2017

Kansela Angela Merkel wa Ujermani amekutana na Waziri Mkuu wa China Li Keqian mjini Berlin kuweka agenda ya mkutano wa mataifa saba yaliyoendelea duniani ya G7 uliopangwa kufanyika Hamburg.

https://p.dw.com/p/2dyJ7
Li Keqiang in Berlin mit Angela Merkel
Picha: picture alliance/AP Photo/M.Sohn

Waziri Mkuu wa China lI Keqiang  Alhamisi (01.06.2017) ametowa wito wa kuwepo kwa juhudi za pamoja kuregeza masharti ya biashara na uwekezaji wakati akiwa katika ziara yake nchini Ujerumani. Ametowa wito huo akiwa katika ziara yake nchini Ujerumani ambako amekuwa na mzungumzo na KanselaAngela Merkrel.

Kutokana na kukabiliwa na hali ya wasi wasi, hisia ya kupinga utandawazi na kuongezeka kwa hatua za kulinda masoko duniani,China na Ujerumani zinapaswa kuendeleza uregezaji wa masharti ya biashara na kurahisisha uwekezaji na kulinda taratibu za Shirikisho la Biashara Dunuiani WTO, Li ametamka hayo wakati wa mazungumzo yake na Kansela Angela Merkel mjini Brerlin.

Kiongozi huyo wa China yuko katika ziara rasmi ya siku mbili kwa mkutano wa kila mwaka kati ya wakuu wa serikali utaratibu ambao umekuwa ukitumika tokea mwaka 2004.

Mazungumzo yao yalikuwa yajikite katika suala la kuwa na ushirikiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili.  Masuala ya tishio la kujitowa kwa Trump katika makubaliano ya tabia nchi ya Paris na sera ya uchumi na biashara ya dunia yana dhima kubwa katika mazungumzo hayo.

Li alipokelewa hapo jana kwa heshima za kijeshi.

Sera ya kigeni

Deutschland Li Keqiang in Berlin
Waziri Mku wa China Li Keqiang na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani wakishuhudiwa kusainiwa kwa mikitaba mjini Berlin.Picha: Reuters/F. Bensch

Inasubiriwa kwa hamu kile kitakachojitokeza katika sera ya kigeni iwe katika masuala ya biashara kwa kuzingatia hatua za Trump kulinda masoko au sera ya tabia nchi. Katika mazungumzo hayo Merkel na Li pia waligusia mkutano wa kilele wa mataifa saba tajiri utakaofanyika katika mji wa Hamburg nchini Ujerumani mapema mwezi wa Julai.

Mkuu wa Biashara wa Ujerumani wa Kamati ya Asia na Pasifiki Hubert Lienhard ameitaka China kutimiza ahadi zake kwa vitendo za kufunguwa masoko ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miongozo na sheria halikadhalika kutendewa haki kwa makampuni ya kigeni wakati wa kutolewa zabuni.

Mashirika ya haki za binaadamu yametowa wito kwa Merkel kumhimiza Li kuchukuwa hatua madhubuti kuboresha haki za binadamu nchini China.Shirika la Amnesty International,la Kampeni ya Tibet ma shirika la waandishi wasiokuwa na mipaka yamemkosowa Rais Xi Jinping kwa kukandamiza kwa makusudi haki za binaadamu.

Umoja wa Ulaya na China pia unatarajiwa kukutana leo hii kwa mkutano wa kilele wa siku mbili kusisitiza kujitolea kwao kwa makubaliano ya Paris ya tabia nchi.

Mwandishi : Mohamed Dahman/dpa/AP

Mhariri:Josephat Charo