Kansela Merkel aitetea serikali kubakia kimya | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.07.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kansela Merkel aitetea serikali kubakia kimya

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametetea msimamo wa serikali yake kubakia kimya kuhusu biashara ya vifaru inayodaiwa kufanyika na Saudi Arabia na iliyozusha mabishano makali nchini humu.

Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) gestikuliert am Donnerstag (09.06.11) in Berlin im Bundestag. Der Bundestag debattiert am Donnerstag ueber die Energiepolitik. (zu dapd-Text) Foto: Axel Schmidt/dapd

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel

Kansela Merkel ameliambia gazeti la Kijerumani, "Mittelbayerischen Zeitung" kuwa kuna sababu nzuri za kuweka siri maamuzi yanayopitishwa katika baraza la kitaifa la usalama. Lakini uwazi unaotakiwa, unapatikana katika ripoti ya biashara ya silaha inayotolewa kila mwaka. Inadaiwa kuwa Saudi Arabia inauziwa vifaru 200 vya chapa ya "Leopard 2".

Vyama vya upinzani vya SPD, Die Grüne na Die Linke vinapinga biashara hiyo vikielezea ukiukaji wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia. Mada hiyo itajadiliwa tena hii leo katika bunge la Berlin. Chama cha Die Linke kimetoa mwito kwa serikali kuzuia biashara hiyo ya vifaru.

 • Tarehe 08.07.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/RYQO
 • Tarehe 08.07.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/RYQO

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com