1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kanisa Katoliki lajadili masuala ya familia na mahusiano

7 Oktoba 2014

Maaskofu wa kanisa Katoliki wameanza majadiliano kuhusiana na suala la ndoa na familia .

https://p.dw.com/p/1DRjS
Vatikan Auftakt Bischofssynode 05.10.2014 Papst Franziskus
Papa Francis akihutubia sinodi ya maaskofu mjini VaticanPicha: Getty Images/F. Origlia

Katika muda wa wiki mbili zijazo maaskofu 191 kutoka duniani kote watajadiliana mbele ya kiongozi wa kanisa hilo papa Francis , vipi kanisa Katoliki kutokana na mabadiliko ya kimaisha wataliangalia suala la familia na vipi wanaweza kutoa msaada .

Suala kubwa linahusiana na familia zinazoishi bila ndoa , watu waliooa na kuolewa baada ya talaka, watu wa jinsia moja wanaoishi pamoja na wale wanaoishi bila ya hati ya ndoa.

Vatikan Auftakt Bischofssynode 05.10.2014
Maaskofu wakiingia katika ukumbiPicha: Getty Images/F. Origlia

Ndoa haivunjiki

Kwa mujibu wa mafundisho ya Kikatoliki ndoa haiwezi kuvunjwa. yeyote atakaye toa neno la kukubali ndoa katika kanisa Katoliki , baada ya kuachana hawezi tena kuoa.

Wakatoliki ambao wameoa tena baada ya kuacha watatupwa nje ya kanisa hilo, mtu ambaye ameajiriwa katika kanisa Katoliki atakuwa yuko katika hatari ya kufukuzwa kazi. Katika hilo kanisa Katoliki pia hapo baadaye halitatikiswa, anasema kadinali George Pell kutoka Australia.

Vatikan Auftakt Bischofssynode 05.10.2014
Kikao cha Sinodi ya maaskofu wa kanisa KatolikiPicha: Getty Images/F. Origlia

"Kutokuvunjika kwa ndoa ni ukweli muhimu katika mafundisho ya mwenyezi Mungu."

Mkutano huu wa maskofu unahusu mvutano huu wa siku nyingi dhidi ya ukweli halisi. Kwa upande mmoja wako makadinali kama Pell, ambao kila mmoja anayejaribu kuleta uwazi kuhusu suala hilo anaonekana kama msaliti kwa mafundisho halisi.

Kwa upande mwingine kuna makadinali kama mwenyekiti wa kamati ya maaskofu wa Ujerumani Reihard Marx . Kadinali huyo kutoka mji wa Munich anatambua , kwamba katika hali halisi Wakatoliki wengi wamejiweka mbali na mafundisho hayo.

Ukweli halisi

"Wengi wanatumia neno ukweli na kisha wanasikia baridi. Kwa hiyo huo si ukweli halisi. Ukweli katika waumini wa Kikatoliki ni katika mtu, ambaye atakuja kwetu . Na uongozi wa kanisa utatafuta njia za kumuelewa, kitu gani mtu huyu Yesu Kristo anataka tumwambie."

Wengi wa maaskofu wa Ujerumani wanaunga mkono kama Reinhard Marx pendekezo la kadinali Walter Kasper, ambae anataka Wakatoliki ambao wamefunga tena ndoa wapewe muda na kusaidiwa na kisha kulipa faini na baadaye warejeshwe kundini.

"Wakati ndoa ya kwanza imevunjika na ndoa ya pili imefungwa bila ya kulipa deni , hapo ni lazima patafutwe njia. Hii sio ndoa mpya ya kanisa. Tunapaswa kuchukua yale mazuri , kwamba hata ndoa ya kiraia itambulike na pia watu wanachokitaka iwezekane kuwarejesha katika kanisa."

Vatikan Auftakt Bischofssynode 05.10.2014 Papst Franziskus und Peter Erdo
Papa Francis mbele ya maaskofuPicha: Getty Images/F. Origlia

Papa Francis kwa kiasi fulani anatambua na kuzikubali hisia za rai hiyo ya Kasper. Kusamehe ndio dhamira kuu ya uongozi wake katika kanisa hilo. Muda mfupi baada ya kuteuliwa kuwa kiongozi wa kanisa hilo ametoa wito mjini Roma , wa kuwa wasemehevu.

Kutokana na hilo wengi wa Wakatoliki walioachana walianza kupata matumaini, kwamba Kanisa linawafungulia mlango. Makadinali kama mkuu wa kanisa la waumini nchini Ujerumani Gerhard Ludwig Müller ama Pell kutoka Australia wanapinga mafundisho hayo.

Maaskofu watakiwa kuwa huru kusema watakalo

Papst Franziskus 05.10.2014
Papa Francis akisalimiana na maaskofuPicha: Reuters/T. Gentile

Papa Francis amewataka lakini maaskofu hao kuwa wakweli na kusema bila woga na uhuru , wakati sinodi hiyo kuhusu masuala hayo nyeti ya mafundisho ya Kikatoliki kuhusu familia ilipofunguliwa mjini Roma siku ya Jumatatu. Papa amejiweka binafsi kama mdhamini wa mkutano huo kwenda kwa njia ya utaratibu maalum.

Mtu hapaswi kusema hatutaki kusema hiki ama kile ama kwasababu tutafikiria kama hivi , tuseme kitu, na muwe huru kusema kitu chochote tunachojisia , akitumia neno la kigiriki la "Parrhesia" likiwa na maana ya kuzungumza bila woga.

Mwandishi: Tilmann Keinjung / Rom / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman