1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kanda ya video yamuonyesha Mjerumani alietekwa nyara

P.Martin19 Agosti 2007

Stesheni binafsi ya televisheni nchini Afghanistan,imeonyesha kanda ya video ya mfanyakazi wa kike wa Kijerumani alietekwa nyara siku ya Jumamosi mjini Kabul.

https://p.dw.com/p/CH9Q
Polisi nchini Afghanistan wakichunguza magari yanayotokea Kabul,wakimsaka Mjerumani alietekwa nyara siku ya Jumamosi
Polisi nchini Afghanistan wakichunguza magari yanayotokea Kabul,wakimsaka Mjerumani alietekwa nyara siku ya JumamosiPicha: picture-alliance/ dpa

Katika kanda hiyo ya video,mfanyakazi huyo wa shirika la Kijerumani linalotoa misaada,“ora international“ ametaja jina lake na kuonyesha kitambulisho chake cha Kijerumani.Mfanyakazi huyo alie na miaka 31 alitekwa nyara katika mkahawa mjini Kabul.

Tume ya dharura iliyoundwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani inafanya bidii ili mfanyakazi huyo apate kuachiliwa huru.Kwa mujibu wa polisi wa Afghanistan,Mjerumani huyo hakutekwa nyara na wanamgambo wa Taliban,bali ni kundi la majambazi lililohusika na uhalifu huo.