1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni kuanza mwisho wa mwezi lakini kuna changamoto

Saleh Mwanamilongo1 Novemba 2018

Raia wengi nchini DRC hasa kwenye maeneo ya vijijni hawajawahi kutumia kompyuta. Tume inayosimamia uchaguzi inakabiliwa na changamoto ya kuwahamasisha wananchi kuhusu uchaguzi kupitia mfumo wa elekroniki

https://p.dw.com/p/37W0o
Demokratische Republik Kongo Wahlmaschine
Picha: Getty Images/AFP/J. Wessels

Kampeni za uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimepangiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu, lakini bado tume ya uchaguzi inakabiliwa na changamoto kadhaa, zikiwemo uhamasishaji wa wananchi kuhusu uchaguzi kupitia mfumo wa elekroniki. Raia wengi nchini humo hasa kwenye maeneo ya vijijni hawaja wahi kutumia kompyuta.

Zikiwa zimesalia wiki tatu tu kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni za uchaguzi, hekaheka zimewakumba hasa wagombea kwenye uchaguzi wa ubunge wa taifa na ubunge wa majimbo ambao wameanza kujitayarisha kuhusu vifaa vya kampeni za uchaguzi. Garama kubwa kwa wagombea ni upatikanaji wa vifaa,wengi wamesafiri hadi Kinshasa au Kampala,Uganda na wengine hadi China.

Vifaa vyote vya uchaguzi kuwasili DRC ifikapo Novemba 10
Vifaa vyote vya uchaguzi kuwasili DRC ifikapo Novemba 10Picha: Getty Images/AFP/J. Wessels

Changamoto nyingine ni kwa tume huru ya uchaguzi ambayo imeandaa upigaji kura kwa matumizi ya mfumo wa elekroniki. Wengi miongoni mwa raia wa maeneo ya mashambani hawaja wahi kuona komputa. Wengine wakaazi wa Kindu tulio kutana nao,wamehoji umuhimu wa kuenda kupiga kura, wakielezea kusikitishwa na wabunge na viongozi waliochaguliwa kabla kutotekeleza ahadi zao.

Tume huru ya uchaguzi imetangaza kupokea nusu ya machines za kupigia kuras. Na ifikapo Novemba 10, vifaa vyote vya uchaguzi vitakuwa vimewasili nchini. Kwa jumla tume huru ya uchaguzi imepanga kutumia komputa laki moja kwa ajili ya upigaji kura wa desemba 23. 

 

Mhariri: Iddi Ssessanga