1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:wakimbizi wamiminika Uganda kutoka Kongo

5 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSU

Shirika la umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR limesema kwamba takriban wakimbizi elfu 10 kutoka mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamevuka mpaka na kuingia nchini Uganda kujiepusha na mapigno yaliyozuka upya kati ya vikosi vya serikali na wanajeshi waasi Mashariki mwa Kongo.

Mashirika ya kutoa misaada yameripoti kuendelea kumiminika wakimbizi kutokana na hali ya wasiwasi iliyopo mashariki mwa Kongo mashirika hayo yanafuatilia kwa umakini za ugavi wa misaada ya kibinadamu.

Afisa wa Uhusiano wa nje wa shirika la umoja wa mataifa UNHCR bibi Roberto Russo amesema.

Ongezeko la wakimbizi linahitaji msaada mkubwa na kwa hivyo amewatolea mwito wafadhili wa kimataifa na wa kibinafsi kutoa misaada kwa ajili ya wakimbizi hao.

Msemaji wa kikosi cha umoja wa mataifa nchini Kongo meja jenerali Gabriel de Brosses amesema kwamba wanajeshi wa serikali wamepelekwa katika eneo la Kivu ya kaskazini.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon ameeleza wasiwasi wake kuhusu mapigano ya mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na amezitaka pande zote mbili kutafuta suluhisho la amani.