1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Mugabe haalikwi mkutano wa jumuiya ya madola

30 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLS

Serikali ya Uganda imesema haitomualika rais Robert Mugabe wa Zimbabwe katika mkutano wa jumuiya ya madola utakaofanyika nchini humo mwezi Novemba.Wizara ya mambo ya nje ya Uganda imesema suala la kualikwa kwa rais Mugabe halina mjadala kwa sababu Zimbabwe ilijitoa kwenye jumuiya hiyo mwaka 2003.

Uanachama wa Zimbabwe katika jumuiya ya madola ulifutwa mwaka 2002 baada ya nchi hiyo kufanya uchaguzi ulioibua utata mwingi na baadae mwaka 2003 nchi hiyo ikajiondoa kwa hiari katika jumuiya hiyo.Hata hivyo nchi nyingi za Afrika wanachama wa jumuiya ya madola wanapinga kutengwa kwa Zimbabwe.