1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampala. Makubaliano ya amani hatarini?

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3B

Waasi nchini Uganda pamoja na serikali ya nchi hiyo kwa pamoja wamekuwa wakikiuka makubaliano ya kusitisha mapigano na kuonekana kama hatua muhimu kuelekea kumalizwa kwa vita vya muda mrefu kabisa barani Afrika.

Mpatanishi mkuu amesema jana kuwa licha ya matumaini kuwa makubalino ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini mwezi wa August yatasaidia kumaliza mapigano yaliyokuwa yakiendeshwa na kundi la waasi la Lord’s resistance Army , LRA , malumbano kati ya serikali na waasi katika muda wa wiki chache zilizopita yametikisa matumaini ya mapema.

Riek Machar , makamu wa rais wa serikali ya Sudan na kiongozi wa kusini mwa Sudan ambaye ni mpatanishi mkuu katika mazungumzo hayo ya amani, amesema pande zote mbili zimevunja makubaliano hayo, baada ya wachunguzi wa binafsi walipothibitisha kuwa karibu wapiganaji 800 wa LRA wameondoka katika vituo vya kujumuika vilivyokubalika chini ya makubaliano hayo.