1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Baada ya mafuriko kitisho cha magonjwa

29 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLl

Nchi za Kiafrika zilizoathirika sana kwa mafuriko mabaya kupata kushuhudiwa barani Afrika,sasa zinakabiliwa na kitisho cha magonjwa ya mripuko. Ugonjwa wa kipindupindu umeshaua watu 68 nchini Sudan.Wasaidizi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wamesema,hadi watu 625,000 huenda wakahitaji misaada ya dharura.Nchini Uganda pia si chini ya watu 400,000 wanahitaji misaada katika maeneo ya mashariki.Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita,kiasi ya watu 300 katika nchi 20 wamepoteza maisha yao na maelfu wengine hawana mahala pa kuishi.