1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamati ya kushughulikia mabadiliko ya Katiba nchini Kenya inapendekeza kusogezwa mbele kwa uchaguzi mkuu

22 Juni 2007

Kamati ya kushughulikia mabadiliko ya Katiba inayosimamiwa na makamu wa rais Moody Awori inapendekeza kusogezwa mbele kwa uchaguzi mkuu.

https://p.dw.com/p/CHCK

Kamati hiyo inapendekeza uchaguzi kufanyika kila alhamisi ya mwisho ya mwezi wa Februari baada ya kila muhula wa miaka mitano kukamilika. Endapo mswada huo utapitishwa bungeni, bunge la sasa litaendelea na shughuli zake mpaka Februari mwaka ujao. Pendekezo hilo ni sehemu ya mswada wa katiba unaolenga kuhakikisha kuwa Bunge linaendeshwa na ratiba maalum. Kwa sasa ratiba ya bunge inaamuliwa na kiongozi wa taifa. Mapendekezo mengine ni suala la uraia kwa wakenya wanaooa na kuolewa na raia wa kigeni. Kamati hiyo inawajumuisha wabunge wa chama tawala, upinzani na mashirika yasiyo ya kiserikali. Uchaguzi mkuu unapangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Mwai Gikonyo anaripoti zaidi kutoka Nairobi.