1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamanda wa majeshi ya Marekani Mashariki ya Kati William Fallon ajiuzulu

Mtullya, Abdu Said12 Machi 2008

Kamanda wa majeshsi ya Marekani katika Mashariki ya Kati William Fallon amejiuzulu.

https://p.dw.com/p/DNBT
Kamanda wa majeshi ya Marekani katika mashariki ya kati William Fallon.Picha: AP


Kamanda wa majeshi ya Marekani katika Mashariki ya Kati Admeli William Fallon amejiuzulu kutokana na kinachoonekana kuwa tofauti kati yake na utawala wa rais G W. Bush juu ya Iran.

Kwa mujibu wa vyombo habari kamanda Fallon anapinga siasa ya utawala wa rais G. Bush juu ya Iran. Kumewapo uvumi katika vyombo vya habari hivi karibuni kwamba utawala wa rais Bush unaanda mashambulio dhidi ya Iran.

Hatahivyo waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amesema hatua ya kamanda Fallon haiashirii mabadiliko katika siasa ya Marekani juu ya Iran.

Akitangaza uamuzi wa kamanda Fallon kujiuzulu waziri Gates amesema hiyo ni hatua sahihi kutokana na tofauti baina yake na utawala wa Marekani zilizojitokeza hadharani.

Voymbo vya habari nchini Marekani vinadai kwamba kamanda William Fallon alikuwa kipingamizi katika mipango ya utawala wa rais Bush juu ya Iran.Lakini wizara ya ulinzi imakanusha madai hayo.Waziri wa ulinzi Gates ameeleza kuwa hakuna tofauti kubwa kati ya admeli  Fallon na utawala wa rais Bush juu ya   Iran. Waziri huyo amesema wazo la vyombo vya habari kwamba kung'atuka   kwa kamanda huyo kunaashiria mipango ya Marekani kuanzisha vita dhidi ya Iran  ni upuuzi.

Hatahivyo katika mahojiano na shirika la televisheni la Aljazeera kamanda Fallon alieleza matumaini kuwa hapatakuwa vita  kati ya Mareekani na Iran. Wadadisi wanasema kauli hiyo iliwaughabisha utawala wa bwana Bush.

Wadadisi wamesema hatua ya kamanda huyo kuondoka, imekuja wakati ambapo utawala wa Bush unaendesha kampeni duniani kote yenye lengo la kuimarisha shinikio dhidi ya Iran kutokana na mpango wa nchi hiyo kurutubisha madini ya uranium .Nchi za magharibi pamoja na  Marekani  zinadai kuwa Iran inaendelea   na mpango huo kwa lengo la kuunda  silaha za nyuklia.Lakini Iran yenyewe imekanusha madai hayo.