1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL.Wapiganaji 50 wauwawa

26 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzJ

Wanajeshi wa muungano wa NATO wamewauwa takriban wapiganaji 50 wa Taliban katika mapigano makali yaliyozuka kusini mwa Afghanistan.

Kikosi cha ISAF pia kimeanzisha uchunguzi kuhusu madai kwamba raia wameuwawa katika shambulio la ndege wakati wa mapambano.

Wanakijiji wa Panjwayi wamedai kuwa takriban raia 60 wameuwawa katika mlipuko wa bomu. Kikosi cha ISAF kimesema kuwa kinasikitishwa na vifo hivyo vya raia.