1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL:Rais Hamid Karzai aponea kuuwawa

Maafisa nchini Afghanstan wamesema wanamgambo wa Taliban wamerusha roketi karibu na uwanja wa shule ambako rais Hamid Karzai alikuwa na mkutano na viongozi pamoja na wakazi kwenye mkoa wa kati nchini humo.

Hata hivyo hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo linalosemekana lilikuwa jaribio la kutaka kumuua rais Karzai.

Shambulio hilo la roketi limetokea huku kukiwa na mapigano na mashambulio ya angani katika eneo la kusini na kaskazini magharibi mwa nchi ambako watu 47 wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Taliban na polisi wawili wameuwawa.

Rais Hamid Karzai alikuwa akitoa hotuba kwa wazee na wakaazi wa eneo la Andar katika jimbo la Ghazni wakati roketi hizo zilipovurumishwa karibu na mahala hapo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com