1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL.Polisi auwawa katika shambulio la kujitoa muhanga

26 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCON

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga amesababisha kifo cha polisi mmoja nchini Afghanistan wakati polisi huyo alipojaribu kumzuia mtu huyo kuingia ndani ya kituo cha polisi.

Mshambuliaji huyo wa kujitoa muhanga alijilipua kwa mabomu aliyokuwa amejizingirisha kwenye mwili wake, watu saba pia wamejeruhiwa katika shambulio hilo katika mji wa Khost mashariki mwa Afghanistan.

Kwa mujibu wa taarifa za jeshi la Marekani takriban raia 200 na wanajeshi kadhaa wa Afghanistan na wale wa kimataifa wameuwawa katika mashambulio ya aina hii.