1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL:Mullah wa kitaleban auawa katika mashambulizi ya anga ya Marekani

Maafisa nchini Afghanistan wamesema kuwa kamanda wa kundi la Taliban aliyehusika na utekaji nyara wa raia 23 wa Korea Kusini mwaka huu ameuawa katika mashambulizi ya anga ya majeshi ya Marekani.

Mullah Abdullah Jan ni miongoni mwa wanamgambo kadhaa wa Taliban waliyouawa katika mashambulizi hayo hapo jana kwenye jimbo la Ghazni.

Kumekuwa na harakati kubwa za kijeshi katika jimbo hilo la Ghazni dhidi ya wanamgambo wa kitaleban toka kuachiwa huru kwa mateka hao wa Korea Kusini mwishoni mwa mwezi uliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com