Kabul.Jeshi la NATO lawauwa watu 55 wanaotuhumiwa kuwa ni wanamgambo. | Habari za Ulimwengu | DW | 31.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kabul.Jeshi la NATO lawauwa watu 55 wanaotuhumiwa kuwa ni wanamgambo.

Jeshi la kulinda amani la NATO limesema kuwa, vikosi vyake huko kusini mwa Afghanistan yamewauwa watu 55 wanaotuhumiwa kuwa ni wanamgambo katika mashambulizi ya saa sita katika jimbo la Zabul.

Aidha mwanajeshi mmoja wa jeshi la kulinda amani nchini Afghanistan ISAF ameuwawa katika mashambulizi hayo.

Shambulio hili limefanywa baada ya lililofanywa mapema siku ya Jumapili ambalo lilipelekea kuuwawa kwa watu 70 wanaoshukiwa kuwa ni wanamgambo baada ya ISAF kukishambulia kituo cha wanamgambo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com