KABUL: Watu 10 wauwawa kwenye shambulio la bomu
23 Januari 2007Matangazo
Watu takriban 10 wameuwawa leo na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la bomu lililofanywa na mtu aliyejitoa mhanga maisha nje ya kambi ya jeshi la shirika la NATO kusini mwa Afghansitan.
Gavana wa jimbo la Khost amenukuliwa akisema kwamba walioathiriwa ni wafanyakazi waliokuwa wakisubiri kwenye kituo cha upekuzi wakitaka kuingia ndani ya kambi hiyo kufanya kazi. Msemaji wa NATO amesema hakuna mwanajeshi aliyejeruhiwa katika hujuma hiyo.