KABUL: Washukiwa kuhojiwa Afghanistan
9 Oktoba 2006Matangazo
Maofisa wa usalama nchini Afghanistan wanapanga kuwahoji washukiwa sita kuhusiana na mauaji ya waandishi wawili wa habari raia wa Ujerumani.
Karen Fischer na Christian Struwe, waliokuwa wakifanya kazi na shirika la habari la Deutsche Welle, walipigwa risasi juzi Jumamosi katika hema lao mkoani Beghlan, yapata kilomita 120 kaskazini mwa mji mkuu Kabul.
Msemaji wa Taliban amesema kundi hilo halikuhusika na mauaji hayo.